Mh. Wangabo ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Parole Mkoa wa Rukwa ambayo hudumu kwa miaka mitatu .
Amesema kuwa wafungwa wengi wanaotoka kwa mpango huo wanakuwa wametumikia kifungo cha zaidi ya miaka minne gerezani na watokapo huwa na ujuzi wa kuweza kujiajiri na kuweza kuendelea kulitumikia taifa katika kukuza uchumi na kuacha kuwa tegemezi katika familia.
Pamoja na hayo Mkuu wa Magereza Mkoa wa Rukwa ACP. Simon Ihunja amezitaja changamoto zinazowakumba wafungwa hao wanapotoka gerezani ni kukosa kuwezeshwa baada ya kutumikia vifungo vyao.