Friday , 2nd Feb , 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Adelardus Kilangi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Dkt. Adelardus Kilangi umeaanza tarehe 01 Februari, 2018.

                                                        Dkt. Adelardus Kilangi

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Kilangi alikuwa Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (St. Augustine University) kituo cha Arusha, na pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta (Tanzania Petroleum Upstream Regulatory Authority – PURA).