Sunday , 13th Mar , 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewathibitisha watendaji wakuu wa taasisi mbili za serikali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu Waliothibitishwa ni Bw. Alphayo Kidata, aliyekuwa Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ambaye anakuwa Kamishna Mkuu wa TRA, na Bw. Valentino Mlowola aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), ambaye anakuwa Mkurugenzi Mkuu wa (TAKUKURU).

Watendaji hawa wamethibitishwa kuanzia leo tarehe 13 Machi, 2016