Friday , 7th Feb , 2014

Rais wa Tanzania Dkt.

Rais wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete leo anatarajiwa kutaja majina ya wajumbe watakaounda bunge la Katiba linalotarajiwa kuanza vikao vyake Februari 18 mwaka huu.

Katika orodha ya wajumbe hao Rais Kikwete ametangaza kuwaacha watu 3,553 miongoni mwa waliopendekezwa huku akiwaonya wanasiasa kuweka mbele maslahi ya taifa na kuacha kutumiwa na vyama vyao.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika mkutano wa baraza la vyama vya siasa, Rais Kikwete amesema majina ya wajumbe wote yatawekwa hadharani baada ya kukamilisha kazi ya kuchambua kwa kushirikiana na Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamedi Shein.

Rais Kikwete amesema watu walioomba kuingia katika bunge hilo ni wengi na haitawezekana wote kuingia hivyo watu 3,553 wataachwa na kuwaomba wasisononeke au wasifikirie vibaya ni kutokana na idadi ya watu kuwa kubwa.