Saturday , 22nd Mar , 2014

Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania amewataka wajumbe wa bunge maalum la katiba kujadili rasimu ya katiba neno kwa neno ili kuona namna ya kuirekebisha katiba hiyo na pale wanapoona kuna vifungu vya sheria visivyo stahili wanawajibu wa kuvifuta.

Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete.

Akilihutubia bunge maalum la katiba mjini Dodoma jana, Rais Kikwete ametumia fursa hiyo kufafanua masuala mbali mbali ikiwemo athari za kuwepo kwa serikali tatu na suala la muungano ambapo amewataka wajumbe hao kuwa makini katika kutoa maamuzi yao juu ya uundwaji wake na kuacha kusikiliza maneno ya kuambiwa na watu kwa lengo la kuyaingiza katika katiba hiyo mpya.

Rais Kikwete amesema ni jukumu la wajumbe hao kufahamu kwamba suala la serikali tatu linahitaji kutazamwa kwa umakini mkubwa na suala hilo ni lazima wajumbe wawe makini kwani litakwamisha baadhi ya maslahi kwa manufaa ya wananchi.