Tuesday , 21st Jun , 2016

Raia wa Uingereza ambaye alijaribu kumpokonya silaha polisi katika mkutano wa Donald Trump Jijini Las Vegas nchini Marekani amesema alikuwa anataka kumpiga risasi muwania urais huyo wa Marekani.

Raia wa Uingereza Michael Steven Sandford akiwa amedhibitiwa na polisi wa Marekani

Muingereza huyo Michael Steven Sandford, 20, hakujibu shtaka linalomkabili wakati alipofikishwa mbele ya Jaji huko Nevada na amerejeshwa rumande hadi hapo kesi yake itakaposikilizwa Julai 5.

Michael Steven Sandford, anashtakiwa kwa kufanya ghasia katika eneo ambalo hakuruhusiwa kuwepo.

Muingereza huyo ameripotiwa kuwa alijaribu kumpokonya silaha polisi, baada ya kusema kuwa alikuwa anataka kupata saini ya Bw. Trump kwenye mkutano wake siku ya jumamosi.