
Naibu kamishna wa Uhamiaji Abbas Irovya akizungumza na waandishi wa Habari
Idara ya Uhamiaji nchini Tanzania imesema jumla ya raia wa kigeni 4,792 wamekamatwa kwa makosa mbalimbali ya kukiuka sheria za uhamiaji nchini kufuatia msako uliofanywa na idara hiyo katika kipindi cha mwezi Januari na Aprili mwaka huu.
Hatua hiyo imefikiwa kufuatiwa msako wa kuwabaini raia wanaoishi nchini Kinyume cha sheria, Akizungumzia hatua hiyo Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji nchini Kamishna Msaidizi Abbas Irovya anasema raia hao wa kigeni wamekamtwa katika mikoa mbalimbali nchini kwa idadi tofauti katika miezi hiyo minne.
Kamishna Msaidizi Irovya amesema raia hao wa kigeni wamechukuliwa hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kurudishwa makwao na wengine kuwafikisha mahakamani.
Raia 132 wamefungwa baada ya kutiwa hatiani huku kesi 383 bado zinaendelea katika Mahakama mbalimbali nchini katika mikoa yote 31 ya Tanzania.