
Prf Mbarawa ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na bodi hiyo kupitia Teknolijia ya video toka mjini Dodoma na kubainisha kuwa TPA inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na wafanyakazi kupeana ajira kindugu, Utendaji usiozingatia matokeo , na mifumo mibovu ya ukusanyaji mapato hali inayopelekea utendaji usiozingatia ufanisi.
Kwa upande wake Mwenyekiti mpya wa bodi hiyo Prf Ignas Rubaratuka amemhakikishia waziri Mbarawa kuwa bodi yake imejipanga kukabiliana na changamoto zote za bandari nchini ili kuwa fursa na kazi hiyo wataifanya kwa weledi mkubwa.
