Kamanda wa Polisi mkoa wa kusini Unguja kamishna msaidzi Juma Saadi
Katika hali ya kushangaza na kushtua Jeshi la Polis mkoa wa kusini Zanzibar limefanikiwa kuzinasa risasi 123 za kivita zilizokuwa ndani ya magazini Nne ambazo zilikuwa ndani ya kisima huku ikiwakamata watu wawili kutokana na kuondoka na risasi hizo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa kusini Unguja kamishna msaidzi Juma Saadi Khamis ambaye alifika kwenye tukio amethibitisha kupatikana kwa risasi hizo amabazo zilikuwa ndani ya magazini Nne na zilikuwa zimezongwa ndani ya majani ya mgomba ambapo wachimba kisima waliokuwa wakikisafisha ndiyo walioziibua na kuzitoa ambapo awali hawakuzielewa kama ni risasi.
Mmoja wa wachimbaji hao aliyefahamika kwa jina la Gefrey Silas amesema wao waliziweka juu na wakaja vijana wawili wakazichukua baadhi yake na ndipo wakatoa taarifa kwa Polisi jamii.
Akitoa maelezo ya ziada kamanda Juma amewataja watu wawili Abdullah Suleiman na Mateo Makungu maarufu dilli wote wakazi wa kizimbani ambao walizichukua na kuzifukia katika eneo lingine huku akithibitisha risasi na magazine zote zimepatikana na upelelezi bado unaendelea huku risasi hizo zikionekana ni za muda.
Hili ni tukio la pili la Polisi kukamata shehena kubwa za risasi za vita katika kipindi cha miezi mitatu ambapo risasi hizo zimekutwa katika shamba linalomilikiwa na mmoja ya mwananchi na eneo hilo halina makazi ya watu isipokuwa walinzi pekee na kisima hicho kimekuwa hakitumiki kwa muda mrefu.