Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala Mary Nzuki
Hatua ya kukamatwa na nyaya hizo imetokana na baadhi ya wasamaria wema kuiarifu polisi baada ya kutilia shaka lori moja lililobeba nyaya hizo katika nyumba ya mkazi huyo na kusafirishwa na ndipo polisi ilipofika na kufanya ukaguzi ikazikuta katika lundo huku mhusika akikimbia na kuacha familia yake.
Meneja wa shirika la ugavi la umeme tawi la Kisarawe Madaraka Marumbo amesema ni wizi mkubwa ambao unashangaza kuona vifaa vilivyokutwa hapo ni vingi vyenye kama ghala huku ikiwa na thamani isiyopungua milioni 100 ambayo vinaweza kupelekwa kwenye mradi wowote.
Mwenyekiti wa mtaa huo wa Nyeburu Hamisi Gea amesema aliitwa na polisi waliokuwa wakitaka kufanya upekuzi na alishangazwa kuona mkazi huyo akiwa na lundo la vifaa hivyo.