Mmoja wa watuhumiwa anashikiliwa na polisi baada ya kutupiana risasi na polisi, huku mtu mmoja mwingine akijisalimisha polisi, kwa mujibu wa twitti ya polisi.
Milio ya risasi ilisikika wakati waandamanaji hao wakiandamana Mjini Dallas, katika maandamano yaliyochochewa na vifo vya Philando Castile huko Minnesota na Alton Sterling huko Louisiana, waliouwawa na polisi kwa risasi.





