Monday , 6th Mar , 2017

Watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wameawa katika mapambano na jeshi la Polisi Mkoani Mbeya, wakati wakiwa katika harakati za kufanya uhalifu.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Emmanuel Lukula

Taarifa iliyotolewa leo na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Emmanuel Lukula, amesema kuwa tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 05.03.2017 majira ya saa 3:30 usiku katika eneo la mlima nyoka, Uyole, Jijini Mbeya katika barabara ya Mbeya/Njombe.

Amesema katika tukio hilo Jeshi la Polisililipambana na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi wanaokadiriwa kuwa watano wakiwa na silaha na kufanikiwa kuwaua majambazi wawili wenye umri wa miaka kati ya 30-35.

Katika tukio hilo silaha tatu zilikamatwa ambazo ni Pistol moja yenye namba 550285 na magobole mawili pamoja na risasi moja ya pistol ambazo zilikuwa zikitumiwa na majambazi hayo.

Majambazi hao walifika katika eneo hilo kwa lengo la kufanya uhalifu ambapo Polisi walipata taarifa na kufika eneo hilo.

Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya kwa utambuzi. ufuatiliaji unaendelea ili kubaini mtandao mzima wa wahalifu hao

Eneo la Mlima Nyoka ni eneo lenye mlima na mteremko mkali hivyo magari hulazimika kupunguza mwendo na kupanda mlima taratibu hivyo wahalifu hutumia nafasi hiyo kudandia magari na kufanya uhalifu.