Monday , 15th Feb , 2016

Maafisa wawili wa polisi waliopatikana na hatia kuhusiana na mauaji ya msichana wa umri wa miaka 14 nchini Kenya wamehukumiwa kifungo cha miaka saba jela kila mmoja.

Veronica Gitahi, aliyekuwa afisa wa uchunguzi wa jinai wa cheo cha inspekta na konstebo Issa Mzee Askari polisi waliohukumia miaka saba kwa mauaji

Maafisa hao Veronica Gitahi, aliyekuwa afisa wa uchunguzi wa jinai wa cheo cha inspekta na konstebo Issa Mzee wamehukumiwa baada ya kupatikana na hatia ya kuua bila kukusudia wiki iliyopita.

Jaji alikataa utetezi wao kwamba walifyatua risasi wakijilinda baada ya kushambuliwa na msichana huyo Kwekwe Mwandaza Agosti 2014 katika eneo la Kinango, Kwale eneo la Pwani ya Kenya.

Familia ya Kwekwe haijaridhishwa na uamuzi huo na mamake marehemu amezimia muda mfupi baada ya hukumu kutolewa na kukimbizwa hospitalini.