Friday , 11th Nov , 2016

Kundi la wataalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa , limelaani machafuko yaliyoambatana na msako wa polisi dhidi ya watu waliokuwa wakiandamana kwa amani katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi.

Polisi nchini Kenya wakimuadhibu muandamanaji.

Wataalam hao wameitaka mamlaka ya nchi hiyo kuchunguza madai ya matumizi ya nguvu kupita kiasi na kukamatwa kiholela kwa waandamanaji na waandishi wa habari na kutaka wote waliohusika kuwajibishwa.

Watu hao walikuwa wakiandamana kupinga madai ya ufisadi unaofanywa na serikali wakati polisi walipotumia mabomu ya kutoa machozi na virungu kuwatawanya ambapo watu kadhaa wameripotiwa kuumia au kuwekwa rumande kufuatia tukio hilo la Novemba 3, mwaka huu.

Wataalamu hao wamesema kuingilia haki ya uhuru wa kuandamana kwa amani ni suala lisilosameheka na hasa pale ambapo waandamanaji wanadai uwajibikaji kutoka kwa serikali.

Polisi wakituliza ghasia nchini Kenya.