Mkuu wa polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam, kamishna wa polisi Suleiman Kova.
Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam, kamishna wa polisi Suleiman Kova amesema Mollel anatafutwa na vyombo vya dola kutokana na kuhusika katika matukio kadhaa likiwemo la wizi wa takribani shilingi milioni 390 zilizoibwa kutoka tawi la benki ya Barclays Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa kamanda Kova, mtuhumiwa huyo ni mume wa meneja wa tawi hilo la Barclays na kwamba uchunguzi wa polisi umebaini kuwa amehusika katika matukio mengi ya uhalifu katika mabenki, yaliyotokea katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.







