
Naomba kuuliza serikali mpango wa kujenga vituo vya polisi 4136 nchi nzima Kituo cha Polisi Kirano na Kabwe vipo kwenye mkakati huo? Ameuliza Mbunge Kessy.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni amesema kwamba vituo hivyo havipo katika orodha iliyotajwa lakini hata hivyo serikali ina mpango wa kukarabati makazi ya askari polisi hivyo itachukua jambo hilo kwa uzito wake.
Aidha Naibu Waziri Masauni amesema kwamba atafanya ziara katika eneo hilo kujionea hali halisi na kushauri kwa kuwa Mbunge Kessy ameeleza kwamba vituo hivyo havina milango ala saruji ni vyema fedha za mfuko wa jimbo zikasaidia kutatua kero hiyo wakati serikali ikitafuta fedha za kuwasaidia askari hao.