Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wakiwemo wanafunzi wa chuo kikuu cha kilimo Sokoine cha mjini Morogoro wamesema chanzo cha tukio hilo ni kukatika mara kwa mara kwa umeme na uliporudi kwa nguvu baadhi ya vifaa vilishika moto na kuanza kuwaka ingawa hakuna madhara kwa wapangaji isipokua vyakula na samani za ndani zimeteketea na kuomba kupewa hifadhi.
Afisa mtendaji kata ya Magadu Haziza Khalfan amesema wanajipanga ili kuona jinsi ya kuwasaidia waathirika wa moto huo kwa kuwapatia hifadhi naye mkaguzi msaidizi wa jeshi la zima moto na uokoaji mkoa wa Morogoro Issa Isandeko amewata wananchi wa mkoa wa Morogoro kutoa taarifa za haraka yanapotokea majanga ya moto.