Sunday , 3rd Jul , 2016

Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage amesema kunauwezekano mkubwa wa nusu ya bidhaa zinazoingizwa nchini kutoka nje ya nchi zinaingizwa nchini zikiwa chini ya viwango.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage amesema kunauwezekano mkubwa wa nusu ya bidhaa zinazoingizwa nchini kutoka nje ya nchi zinaingizwa nchini zikiwa chini ya viwango kwa kuwa kumekuwa na malalamiko mengi yaubovu wa bidhaa hizo kutoka kwa watumiaji wake.

Mhe. Mwaijage ameyasema hayo wakati akizungumza na East Africa Radio na kuongeza kuwa katika kupambana na bidhaa hizo hatari ambazo tayari zimeingizwa sokoni kwa ajili ya matumizi, kwanza wameendelea kutoa elimu kwa walaji hasa katika maeneo yasiyofikiwa kwa uraisi na vyombo vya habari na amewataka wanachi kutoa ushirikiano wa kuwakamata watuhumiwa ambao wanaingiza bidhaa hizo nchini kinyume cha sheria.

Amesema serikali kupitia wizara hiyo wameanzisha utaratibu maalum ambao wanawapeleka wataalamu kwenye viwanda vya nje ambavyo wanaleta bidhaa zao nchini kwa ajili ya kukagua njia na taratibu za ubora zinavyofanyika hadi kuwafikia walaji wa Tanzania.

Amesema katika kuhakikisha Tanzania inapata viwanda zaidi na kupata bidhaa zenye ubora kiafya wameamua kuweka nguvu nyingi katika ukaguzi wa viwanda vya ndani na vya nje ili kuhakikisha afya za watanzania zinaimarika.