Tuesday , 5th Jul , 2016

Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage amewataka watanzania kuthamini bidhaa za ndani kwani zinadumu kuliko baadhi ya bidhaa kutoka nje ya nchi ambazo baada ya muda mfupi zinaharibika kwa kukosa ubora.

Mwijage ameyasema hayo alipokuwa akizungumza kwenye kipindi cha Supa Mix kinachorushwa na East AfriCA Radi Jijini Dar es salaam.

‘’Kuna nguo nyingine ukinunua hazidumu kabisa mfano ukichukua mashati unaweza fua baada ya muda mfupi yanakuwa kama chandarua wakati na viatu baada ya muda mchache vinaharibika na watanzania huwa tunatembea kilomita nyingi, hivyo bidhaa za ndani ni suluhisho’’ Amesema Mwijage.

Aidha waziri amesisitiza mamlaka zinazohusika na kuhakikisha ubora wa bidhaa nchini vifanye kazi yake ipasavyo na wasiogope mtu yeyote hata waambiwe mzifo ni wa nani wasimamie sheria za utawala ili kumlinda mlaji hii itasaidia pia bidhaa za ndani kuuzika.