Wednesday , 20th May , 2015

Serikali mkoani Njombe inatarajia kufanya ukarabati wa barabara zake na kutengeneza sehemu ya kupita watembea kwa miguu katika eneo la umbali wa mita 700 kwa lengo la kupunguza ajali katika maeneo ambayo barabara ni hatarishi.

Picha za hali ya Barabara ya Makete -Njombe eneo la Igagala.

Akizungumzia ukarabati huo na matengenezo ya barabara za mkoa wa Njombe kaimu meneja wa Tanroad Eng. Kipembawe Msekwa amesema kuwa ukarabati huo utalenga kuboresha barabara na kuondokana ajali kwa kuwatenga watembea kwa miguu na magari.

Amesema kuwa wameamua kuanza na sehemu hiyo kutokana na kuwapo kwa ajali nyingi zinazo sababishwa na barabara kuwa nyembamba kwa wapita kwa miguu.

Amesema kuwa barabara ya watembea kwa miguu ambayo imeanza kujengwa itajengwa kwa kutumia vitofari vya block kwa eneo lote na kuwa itakuwa ni kwa watembea kwa miguu pekee na sio baiskeli wala pikipiki.

Ameongeza kuwa ukarabati kwa mkoa mzima Tanroad inatarajia kutumia Bilioni 1.063 kwa mwaka huu wa fedha na wakandarasi wapo tayari kuanza kazi.

Aidha kwa upande wa wananchi mkoani Njombe wamesema kuwa ujenzi huo utakuwa msaada kwao kwa kuwaepusha na ajali na wengine wamelalamikia kutolewa katika eneo la hifadhi ya barabara ambako unapita ujenzi wa barabara ya watembea kwa miguu.