Mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo,(CHADEMA) chini ya Mwamvuli wa UKAWA, Waziri Mkuu wa zamani Mh. Edward Lowassa
Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu ya kuwania nfasi hiyo jana katika ofisi za tume ya Taifa ya Uchaguzi Nec katika ofisi za CHADEMA, Mh. Lowassa atawasaidia vijana hasa ukizingatia mwaka huu ni asilimia 72 ndio waliojiandikisha katika kupiga kura.
Mh. Lowassa ameongeza kuwa Serikali ya CCM imeshindwa kutatua kero mbalimbali na kusababisha maisha kuwa magumu kutokana na kupanda bei kwa bidhaa muhimu zinazotumiwa na wananchi wa hali ya chini kama Majani ya chai,Chumvi, Mafuta, Mchele, Sukari, Mafuta ya taa N.k.
Kwa upande wake Mgombea Urais kwa tiketi ya CUF akiwa chini ya Mwamvuli wa UKAWA kwa upande wa Zanzibar Mh. Maalim Seif Sharrif Hamad amewataka vijana kujitokeza kwa wingi katika siku ya kupiga kura ili kutimiza lengo la kukitoa chama tawala Madarakani.
Nao Viongozi wanaounda umoja huo akiwemo Mh. James Mbatia amesema Umoja huo umejiandaa kuongoza nchi kwa amani na Utulivu hivyo kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi huku Dk. Makaidi akiwataka CCM ,kukubali matokeo mapema na wananchi waipigie Ukawa ili kuiondoa CCM, Madarakani.