Thursday , 27th Oct , 2016

Nigeria inakabiliwa na mgogoro mbaya kabisa wa kibinadamu barani Afrika. Kauli hiyo imetolewa na naibu mratibu wa masuala ya kibinadamu na mratibu wa shirika la OCHA nchini humo Peter Lundberg.

Wakimbizi wa Nigeria kutoka jimbo la Borno wakiwa kambini

 

Hivi sasa watoto takribani laki nne wanakabiliwa na njaa na raia wanakabiliwa na ukosefu wa maji safi, huduma za afya, ulinzi, elimu na hawana uhakika wa chakula.

Amesema jimbo lililoathirika zaidi ni Borno ambako machafuko ya kundi la Boko Haram yamezidisha madhila kwa wananchi. Jumuiya ya kimataifa na serikali ya Nigeria vinajitahidi kutoa msaada lakini OCHA inasema bado hautoshi.

Mpango wa usaidizi wa kibinadamu kwa mwaka 2016 nchini Nigeria unaohitaji dola milioni 484, hadi sasa umefadhiliwa kwa chini ya asilimia 37