Saturday , 4th Jun , 2016

Nguli Bingwa wa zamani wa dunia kwa mchezo wa ngumi za kulipwa uzito wa juu Muhammad Ali amefariki dunia akiwa na umuri wa miaka 74 katika Hospitali ya Phoenix katika jimbo la Arizona ambako alikuwa amelazwa tangu alhamisi.

Bingwa huyo wa zamani wa dunia amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya kiharusi kwa miaka 32 na msemaji wa familia hiyo amesema mazishi yake yatafanyika nyumbani alikozaliwa huko Louisville, Kentucky.

Mohamed Ali ambaye alikuwa akiitwa Cassius Marcellus Clay, aliingia katika ulimwengu wa masumbwi baada ya kushinda medali ya dhahabu katika michuano ya Olimpiki mwaka 1960 uzito wa light-heavyweight huko Roma.

Mwaka 1964 nguli huyo alishinda ubingwa wa dunia baada ya kumpiga Sonny Liston na baadae kuunyamua ubingwa wa dunia mara tatu katika viindfi tofauti alijiuzuru mcgezo huo mwaka 1981 akiwa ameshinda mapigano 56 kati ya mapigano 61.