Mkurugenzi wa NEMC, Bonaventure Baya,
Akizungumza na wakuu wa mikoa wa Kanda ya Ziwa Wakuu wa wilaya ya Mwanza na Maafisa wengine Mkurugenzi wa NEMC, Bonaventure Baya, amesema kati ya miradi 200 iliyokaguliwa katika kanda ya ziwa miradi 86 inatekelezwa bila yakuwa na vyeti vya mazingira.
Akizungumka katika Kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela, amelitaka baraza hilo kurahisisha hatua za upatikanaji wa vibali vya mazingira kwa wawekezaji ili kuepuka lawama za wao kuwa kikwazo cha wawezezaji hao kufuata sheria za baraza hilo.
Nae Mkuu wa Mkoa Simiyu Anthony Mtaka ameishauri NEMC, kusambaza elimu ya mazingira kwa wadau ikiwemo wawezekaji ili kuondoa malalamiko ambayo yanatolewa juu ya baraza hilo ambapo inawezekana malalamiko hayo ni kutokana na ukosefu wa elimu.
Akijibu tuhuma za kuwepo urasimu katika utoaji wa vibali vya tahmini ya athari ya Mazingira katika miradi ya uwekezaji nchini Mwanasheria wa NEMC, Manchari Heche Suguta amesema hatua zilizowekwa zote zipo kwa mujibu wa sheria.