Saturday , 26th Mar , 2016

Naibu waziri ofisi ya makamu wa Rais anaeshughulikia Mazingira Mh. Luhaga Mpina ametoa siku saba kwa Baraza la hifadhi ya mazingira nchini NEMC

Naibu waziri ofisi ya makamu wa Rais anaeshughulikia Mazingira Mh. Luhaga Mpina ametoa siku saba kwa Baraza la hifadhi ya mazingira nchini NEMC, Mamlaka ya safi na taka Dawasa kuhakikisha wanachukua hatua kwa viwanda vinavyotirisha maji machafu katika mifereji inayopita maji ya mvua.

Kauli hiyo ya Mh. Mpina ameitoa leo jijini Dar es salaam mara baada ya kushiriki zoezi la usafi wa mazingira katika eneo la TPDC huko Mikocheni kwa warioba hilo na kubaini kuwepo kwa viwanda vinavyotumia mifereji ya kupitishia maji ya mvua kuitumia mifereji hiyo kwa kupitishia maji machafu yanayotoka viwandani.

"Na hawa watu wengine wenye makampuni na wenye viwanda hakikisheni mamlaka husika zinafuatilia hili suala kwa kipindi cha wiki mbili na baada ya hapa nitarudi kuja kuangalia kama tatizo hili bado linaendelea" alisema Mpina

Amesema hali hiyo haiwezi kufumbiwa macho kwakuwa madhara yake ni makubwa kwa wakazi waishio maeneo ya karibu na mifereji hiyo ikiwemo kuongeza kasi ya milipuko ya magonjwa ukiwemo ugonjwa wa kipindupindu.