Baraza hilo limesema kuwa nchi kwa sasa inakabiliwa na tatizo la kuzagaa kwa vyeti bandia, hivyo limewataka waajiri nchini kote kushirikiana na baraza hilo kutaka kupeleka vyeti vya waajiriwa kwa ajili ya kukaguliwa.
Mkuu wa Idara ya Utawala na Fedha NECTA Bw. Daniel Matie ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwa lengo la kuelezea mafanikio na changamoto zinazolikabili baraza hilo.
Bw. Matie amesema ili kufanikisha kupungua kwa tatizo la vyeti bandia nchini waajiri wanayo nafasi kubwa ya kushirikiana na NECTA katika ukaguzi wa vyeti ili kuchukua hatua za haraka kwa wale watakaobainika wanafanya kazi kwa njia ya kughushi vyeti.