Wednesday , 3rd Jun , 2015

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Jaji Damian Lubuva amekemea tabia ya baadhi ya vyama vya siasa kuingilia majukumu ya tume hiyo katika zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la mpiga kura

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Jaji Damian Lubuva amekemea tabia ya baadhi ya vyama vya siasa kuingilia majukumu ya tume hiyo katika zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la mpiga kura na kuligeuza kuwa ajenda ya kisiasa kinyume na sheria inayoelekeza kuwa tume hiyo ni huru na haaingiliwi.

Jaji lubuva anatoa kauli hiyo wakati akielezea taarifa ya mwenendo wa zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu kupitia mashine za kielectronic za bvr ambapo amesema tume inasikitishwa na baadhi ya vyama vya siasa kuingilia mchakato wa uandikishaji huku vikijua wazi kuwa kufanya hiyo ni kukiuka sheria sambamba na kutoa taarifa zenye upotoshaji kwa umma kuhusu zoezi hilo.

Jaji Lubuva pia akatoa ufafanuzi kuhusu mkanganyiko uliojitokeza kuhusu wanafunzi wa vyuo ambao katika daftari la kudumu wamejiandikisha vyuoni na wakati wa kupiga kura huenda zoezi hilo ilikawakuta nje ya vyuo ambapo amesema kuwa endapo hali hiyo itajitokeza taarifa zao zitabadilishwa kwenye eneo husika wakati wa zoezi la uhakiki wa daftari la awali

kwa upande wake afisa wa tume hiyo Athumani Masesa akizungumzia sheria inasemaje juu ya wafungwa na mahabusu kujiandikisha na hatimaye kupiga kura amesema sheria haitambui namna ya kuwafikia watu hao ambapo pia EATV imezungumza na baadhi ya wanasiasa na kukanusha madai ya kuingilia majukumu ya tume bali hawana imani na maofisa wanaosimamia zoezi hilo.