Thursday , 30th Jul , 2015

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa itaongeza muda wa siku nne tu wa kuandikisha wapiga kura kwa wakazi wa Dar es Salaam, baada ya muda wa awali wa tarehe 31, kumalizika.

Akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema kuwa hataweza kuongeza muda wa zaidi ya siku nne kwa kuwa ratiba zitaingiliana hivyo amewataka wananchi ambao bado wajajiandikisha mpaka sasa kutumia siku hizo nne kjiandikisha .

Aidha, Jaji Mstaafu Lubuva amesema mpaka sasa watu zaidi ya milioni 18 na laki saba wameandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa njia ya mfumo wa kielektroniki BVR kwa nchi nzima huku lengo likiwa ni kati ya milioni 23 na 24..