Tuesday , 24th Mar , 2015

Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania (NEC) leo imesema inawasiwasi na zoezi la kura ya maoni ya Katiba inayopendekezwa kuahirishwa kutokana na kusuasua kwa mwenendo wa uandikishwaji wa daftari la kudumu la mpigakura linaloendelea mkoani Njombe.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Njombe Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema kuwa kura ya maoni ya Katiba mpya inayopendekezwa huenda isifanyike mwishoni mwa mwezi Aprili na kusogezwa mbele ili kukamilisha uandikishwaji wapiga kura.

Jaji Lubuva amesema zoezi la uandikishwaji linavyoendelea katika Mkoa wa Njombe litaenda hadi Aprili 15 na ratiba itatolewa baada ya kukamilika kwa mkoa wa Njombe na itapangwa kutokana na vifaa vitakavyo kuwepo.