Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Mwenyekiti Tume hiyo Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema uandikishaji huo umevuka lengo na kusema kuwa watu walioandikishwa ni sawa na Asilimia 101.2 ya watu wote.
Lubuva amesema hadi kufikia Agost nne Wilaya ya Kinondoni imeandikisha watu 1,157,142 sawa na aslimia 105 wakati makadirio yalikuwa ni watu 1,101,565, Temeke watu 886,564 swa na asilimia 98.9 na Ilala ni 886,564 sawa na asilimia 98.9
Kwa mujibu wa Taarifa hiyo inasema uwekaji wazi wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa mikoa iliyokwishapokea daftari utaanza agost saba na utadumu kwa siku tano katika kila mkoa.
Amesema lengo la uwekaji wazi wa Daftari hilo ni kuhamisha taarifa za wapiga kura waliohama toka kata au jimbo,kutoa kadi kwa wapiga kura waliopoteza kadi zao na kuhakiki kama kila mpiga kura taarifa zake zipo kwenye daftari hilo.