Kiongozi Mkuu wa dini ya kiislam wa madhebu ya Shia, ithana Sharia, Sheikh Hemed Jalala
Wito huo umetolewa na Kiongozi Mkuu wa dini ya kiislam wa madhebu ya Shia, ithana Sharia, Sheikh Hemed Jalala wakati akiongea na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam alipozungumzia mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Sheikh Hemed pia amesema waislam waendelee kutumia mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kudumisha amani na utulivu nchini lakini uwe mwanzo wa mabadiliko ya amani ya kweli kwa maendeleo ya taifa la Tanzania
Aidha Sheikh Hemed pia amaetumia fursa hiyo kulaani vikali vitendo vya mauaji ya waumini wa kiislam kwenye nyumba ya ibada Jijini Mwanza pamoja na watu nane waliouwa mkoani Tanga na kusema kuwa jambo hilo kamwe halikakubali kwenye Ardhi ya Tanzania yenye amani