Mkuu wa Tabora Aggrey Mwanri,
Mwanri ametoa amri ya kuwasaka na kuwakamata wanawake wote waliovamia katika miji ya Igunga na Nzega ambayo ipo katika barabara kuu ya Singida na Shinyanga pamoja na wale wote watakaokutwa wanatumia vileo nyakati za kazi.
Mhe. Mwanri amesema kuwa biashara hiyo ya Ngono na vileo nyakati za kazi inatishia usalama wa afya na utilivu wa watu wa Mkoa wa Tabora ikiwemo kurudisha nyuma maendeleo ya Mkoa.
Akizungumza na Wakazi wa Mji wa Igunga na Nzega, Mhe, Mwanri amesema kuwa wanawake hao wamevamia katika miji hiyo kwa wingi kutokana na miji hiyo kuonekana kuchanganya kibiashara.