Tuesday , 19th Jan , 2016

Jeshi la polisi mkoani Mbeya linamshikilia mwanamke mmoja Nuru Ismail (31) mfanyabiashara wa jijini Dar es salaam akiwa na madawa ya kulevya aina ya bhangi uzito kilo 7 na gramu 100 zikiwa zimehifadhiwa kwenye mabegi ya nguo.

Mtuhumiwa huyo amekamatwa mpakani mwa Tanzania na Zambia katika mji mdogo wa Tunduma wilaya ya Momba mkoa wa Mbeya.

Mtuhumiwa alikuwa akitokea nchini Afrika ya kusini akiwa na hati ya kusafiria (Passport) namba AB.767234 iliyotolewa jijini Dar tar 21/10/2015 akiwa kwenye basi lenye namba T595 BPR kampuni ya Falcon lililokuwa likitokea Lusaka kwenda Dar es salaam.

Aidha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna mwandamizi wa Polisi Ahmed Msangi ameitaka jamii kuacha kutumia madawa ya kulevya kwani ni hatari kwa afya zao na ni kinyume cha sheria.