Thursday , 19th Feb , 2015

Mwakilishi wa jimbo la Magomeni Zanzibar Mh. Salmin Awadh amefariki ghafla akiwa kwenye kikao cha CCM Zanzibar.

Marehem Salmin Awadh enzi za uhai wake

Sababu ya kifo chake bado haijafahamika hadi sasa na maziko yamepangwa kufanyika kesho Februari 20 katika kijiji cha Makunduchi, mkoa wa Kusini Unguja.

Marehem Salmini Awadhi licha ya kuwa mwakilishi wa jimbo hilo kwa zaidi ya miaka 9 tangu mwaka 2005, alikuwa ni mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM, na moja kati ya viongozi waandamizi wa CCM visiwani Zanzibar.

Alizaliwa Tarehe 26 June mwaka 1958 na amewahi kutumikia jeshi la wananchi wa Tanzania kati ya mwaka 1976 na 1986, na mpaka mauti yanamkuta akiwa na umri wa miaka 56 alikuwa ni Makamu mwenyekiti wa bodi ya gazeti la Zanzibar Leo.