Kwa mujibu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa mvua hizo zilianza kunyesha juzi na jana zimesababisha nyumba nyingi kubomoka na kusababisha Zaidi ya watu 300 kukosa makazi.
Kamati hiyo ikiongozwa na diwani wa kata hiyo pamoja na kamanda wa polisi wa wilaya, wamesema hatua za haraka zilizofanyika na kuwachukua waathirika wa janga hilo na kuwaweka katika shule moja huku hatua nyingine za kimsaada zikiendelea kufanyika ili kuepuka madhara zaidi.
Aidha Kamati hiyo imetoa tahadhari kwa wakazi wa mkoa huo waliojenga mabondeni wahame ili kuepuka madhara zaidi kutokana na watabiri wa hali ya hewa kueleza kuwa mvua hizo zitaendelea kunyesha.