Thursday , 5th Nov , 2015

Takribani watu 360 katika kata ya Kigwe Wilayani Bahi mkoani Dodoma wamekosa makazi baada ya nyumba zao 96 kuezuliwa mapaa kutokana na mvua kubwa iliyoambatana na upepo kunyesha Novemba 2 mwaka huu.

Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma, Francis Monga

Akizungumza na waandishi wa habari Ofisa Mtendaji wa kata ya Kigwe, Mgwala Songola amesema kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Novemba 2 mwaka huu, baada ya mvua kubwa iliyoambatana na upepo kunyesha Wilayani hapo.

Amesema mbali na nyumba hizo kuezuliwa na upepo mkali pia imeharibu na kuezua mabati katika nyumba za walimu, kanisa, zahanati pamoja na ofisi ya serikali ya kijiji hicho.

Akizungumzia tukio hilo Khalima Husein ambaye ni walimu wa shule ya sekondari Kigwe amesema nyumba za waalimu zimeezuliwa na upepo na kusababisha walimu kuishi katika mazingira hatarishi.

Kutokana na hali hiyo mwalimu hiyo amesema mpaka hivi sasa wamekuwa wakiishi kwa wasiwasi na kushindwa kwenda darasani.

Pamoja na hali hiyo kujitokeza mkuu wa wilaya hiyo Francis Monga hakuweza kupatikana ili kuelezea ni hatua gani mpaka sasa zinazofanyika kwa ajili ya kuwanusuru wahanga hao.