Monday , 30th Mar , 2015

Mvua  iliyoambatana  na  upepo  mkali wilayani  Arumeru    mkoani   Arusha   amesababisha  maafa  makubwa   yakiwemo  ya  kuharibu   hekari  125  za  migomba.

Mvua  iliyoambatana  na  upepo  mkali  iliyonyesha  katika  kata  za  Nguandua  na  Ambureni  wilayani  Arumeru    mkoani   Arusha   imesababisha  maafa  makubwa   yakiwemo  ya  kuharibu   hekari  125  za  migomba  , kuezua  nyumba  na  kuangusha  idadi  kubwa  ya  nguzo  za  umeme na  wananchi   wa   zaidi  ya  kaya  500   wanahitaji  msaada  wa  haraka  ukiwemo  wa  chakula.

Baadhi  ya   wananchi  waliopatwa  na maafa  hayo   wamesema mvua hizo zilizoanza  majira  ya saa  kumi  jioni  ya  siku  ya  Jumapili zilinyesha  kwa  muda  mfupi  wa  dakika zisizozidi  45  pia  zimeangusha idadi  ku bwa  ya miti  kubomoa  nyumba   na  baadhi ya vyanzo  vya  maji   na  wameiomba  serikali  kuwasaidia.

Mkuu   wa  mkoa  wa  Arusha bw  Felix  Ntibenda   na timu  ya  kitengo  cha  maafa   amewatembelea  wananchi  hao    na   amemtaka   mkuu   wa wilaya kushirikiana  na  viongozi  wa  kata  na  vijiji  kufanya tathimini   na  kutoa  taarifa  haraka  ili  serikali   iweze  kuchukua  hatua  .  

Mkuu   wa wilaya  ya  Arumeru  Hasna  Mwilima   amesema  hatua  za  awali  zimeshachukuliwa   ikiwemo     ya  kuwaarifu   watendaji  wa  TANESCO  kuzima   umeme     kazi  ambayo    meneja  wa  shirika  hilo kituo  cha Usariver  amesema   wameshaifanya  na  wanaendelea   kusimamisha   nguzo  zilizoanguka  .

Kufuatia  maafa  hayo  mkuu  wa  mkoa  Ntebenda   amewataka    wananchi  wanaoishi  mabondeni   kuchukua  tahadhari  za  kuwawezesha  kuepukana  na  madhara yanayoweza  kusababishwa  na  mvua  zilizoanza  kunyesha  na pia  amesisitiza  umuhimu  wa  wananchi  kutumia  mvua  hizi   kupanda  miti