Tuesday , 7th Jun , 2016

Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mtwara (MTPC), kimeiomba wizara ya habari,utamaduni, sanaa na michezo kuwashinikiza waajiri kuwapatia mikataba waandishi ili kulinda masilahi yao na kutatua baadhi ya changamoto za kimkataba wanazokabiliana nazo

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel.

Mwenyekiti wa chama hicho, Hassan Simba, amemweleza katibu mkuu wa wizara hiyo, Prof. Elisante Gabriel kuwa changamoto nyingine wanazokabiliana nazo ni pamoja na waandishi kutokuwa na vitambulisho maalumu (Press Cards) kutoka wizara ya habari vitakavyowawezesha kufanya kazi zao mahala popote nchini.

Aidha, Simba amemshukuru katibu mkuu huyo ambaye amefanya ziara ya kikazi mkoani, kwa kuwapatia msaada wa iPad moja kwa ajili ya kurahisisha mawasiliano baina ya chama hicho na wizara kwa kueleza masuala mbalimbali kwa ajili ya kuboresha tasnia ya habari.

Kwa upande wake, katibu mkuu huyo ambaye ziara yake imelenga kupokea changamoto na kupata maoni juu ya wizara hiyo kutoka kwa wadau mbalimbali wakiwamo wanahabari ambao aliwatembelea katika ofisi yao, ameahidi kwenda kuyafanyia kazi mapendekezo yote yaliyowasilishwa kwa kuyafikisha kwa waziri mwenye dhamana Mhe. Nape Nnauye

Sauti ya Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel
Sauti ya Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mtwara (MTPC), Hassan Simba,