Akithibitisha tukio hilo OCPD wa Eldoret Mashariki Bw Richard Omanga, amesema kuwa Andrew anatuhumiwa kumuua baba yake kwa kumkata kichwa kwa kutumia shoka, baada ya kukataa kumpa kondoo wa familia ili alipe mahari kukomboa mtoto wake wa kiume aliyempata nje ya ndoa.
“Marehemu alikataa kumpa mwanawe kondoo kwa sababu hakujua alikuwa amezaa mtoto nje ya ndoa kama alivyodai. Mshukiwa alikasirishwa na msimamo wa baba yake ndipo alimvamia baba yake akiwa chumbani mwendo wa saa moja, akamkatakata kwa shoka,” alisema OCPD Omanga.
Mtuhumiwa huyo kwa sasa anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Naiberi akisubiri kufunguliwa mashtaka baada ya uchunguzi kukamilika.






