Thursday , 24th Dec , 2015

Serikali imemsimamkisha kazi Mtendaji Mkuu wa mradi wa mabasi yaendayo kasi (DART), Bi. Asteria Mlambo kupisha uchunguzi dhidi ya ukiukwaji wa sheria ya manunuzi katika mradi huo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mheshimiwa George Simbachawene akizungumza na Wanahabari kuhusu kumsimamisha kazi Mtendaji Mkuu wa DART, Bi. Estaria Mlambo kuanzia tarehe 23.

Akiongea na waandishi wa Habari jana Waziri wa Ofisi ya Rais,TAMISEMI,George Simbachawene amesema sababu ya kusimamishwa kwake ni kushindwa kuzingatia sheria ya manunuzi ya umma wakati wa kumpata mtoa huduma katika kipindi cha mpito.

Aidha Mh. Simbachwene amesema kuwa pia mtendaji mkuu huyo ameshindwa kuchukua hatua hata pale alipoabaini mtoa huduma ya mptio amekiuka masharti ya mkataba.

Tatizo jengine amesema ni kufanya manunuzi makubwa pasipo kuishirikisha Bodi ya Usharuri ya Dart.

Katika hatua nyingine Waziri huyo amemuagiza katibu mkuu Tamisemi kuendelea na taratibu za kinidhamu dhidi ya mtendaji mkuu huyo pamoja na baadhi ya watumishi walioshindwa kumshauri mtendaji huyo.