Thursday , 14th Jul , 2016

Serikali ya Tanzania imesema mswada wa sheria wa huduma kwa vyombo vya habari utaanza upya na kuwashirikisha wadau wa habari ili kuobresha na kuwa na faida kwa pande zote.

Naibu waziri wa Habari, Sanaa, Utamuduni na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura.

Naibu waziri wa Habari, Sanaa, Utamuduni na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura amesema hayo jana Jijini Arusha wakati akizungumza na wanamichezo, Wasanii na Waandishi wa habari jijini humo.

Mhe. Wambura amesema kuwa waandishi wa Habari wanamatatizo mengi yanayofanana kwa nchi nzima hivyo mswada huo utaweza kutatua matatizo yanayowakabilika katika utendaji kazi wao.

Naibu Waziri huyo ametumia fursa hiyo kuwataka waandishi wa habari kufanya kazi kwa kuzingatia weledi na kutanguliza uzalendo wanapofanya kazi zao ili kuipa jamii kile kinachostahiki.

Aidha Mhe. Wambura amewataka waandishi wa habari kujiendeleza kielemu ili mswada huo utakapopitishwa ili waweze kupata maslahi mazuri yatakaowawezesha kupata ari ya kufanya kazi