Saturday , 21st Feb , 2015

Serikali ya Tanzania likiwemo jeshi la polisi nchini imetakiwa kuwa na msimamo thabiti wa kukomesha kabisa mauaji ya watu wenye ALBINISM kwa kuwa vitendo hivyo ni vinakwenda kinyume na haki za binadamu na ni ukatili usiokubalika katika jamii yoyote.

Alex Msama

Ushauri huo umetolewa leo jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka Bw. Allex Msama mara baada ya kutoa msaada wa vitu mbali mbali ikiwemo vyakula kwa vituo vitano vya watoto yatima vilivyopo jijini Dar es salaam.

Bw. Allex amesema serikali pamoja na jeshi la polisi imefika wakati kuona kwamba mauaji hayo ya watu wenye ALBINISM yanaitia aibu nchi ndani na nje kwa kuwa ni jambo la kushangaza kuona kwamba kila inapokaribia uchaguzi mauaji hayo ndio yanajitokeza kwa kasi.

Amesema inasikitisha kuona hakuna jitihada za kuridhisha zinazochukuliwa na serikali huku wauaji hao wakiwa bado wamebaki mtaani wakati familia za watu wenye ALBINISM zikiachwa na hudhuni kubwa kutokana na kupoteza ndugu zao.