
Hayo yamethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Ulrich Matei na kusema kukamatwa kwa mtuhumiwa Mabula ni kufuatia matukio kadhaa ya aina hiyo yaliyo ripotiwa kutokea katika maeneo tofauti ya mji huo.
Kamanda Mtei amesema baada ya kupata taarifa, jeshi hilo kwa kushirikiana na timu ya wataalam wa makosa ya mitandao pamoja na Kikosi cha kupambana na ujambazi wakafanikisha kupatikana kwake ambaye baada ya mtuhumiwa kuhojiwa alikiri kuhusika matukio hayo na kudai anafanya hivyo kwa lengo la kujipatia fedha.
Kwa upande mwingine, Jeshi hilo linawashikilia watu watatu ambao ni vinara wa matukio ya utapeli pamoja na wizi kwa njia ya mtandao wakiwa na simu 9 pamoja na line 57 za mitandao mbalimbali zinazotumika kufanya utapeli.
Kwa habari kamili msikilize hapa chini Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Ulrich Matei.