Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto nchini Tanzania imesema bado Halmashauri za wilaya za Morogoro na Manyara zinaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa wa kipindupindu katika kipindi cha wiki noja iliyopita.
Akiongelea hali ya ugonjwa huo nchini hii leo jijini Dar es salaam, Kaimu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Michael John amesema ugonjwa huo bado una idadi kubwa ya wagonjwa ukilinganisha na halmasauri nyingine nchini.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Huduma za Afya wa wizara hiyo, Dkt. Neema Rusibamayila akizungumzia hali ya ugonjwa huo Mkoani Dodoma juu ya taarifa ya kuwepo kwa ugonjwa huo katika hospitali ya wagonjwa wa akili ya Mirembe amesema hawana uhakika kutokana na kupokea taarifa za halmashauri pekee.
Naibu katibu mkuu wa wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Deo Mtasiwa amesema tayari halmashauri zote nchini zimetakiwa kufanya jihitada za kukabiliana na kuongezeka kwa wagonjwa