Saturday , 26th Apr , 2014

Wodi ya watoto wenye saratani za aina mbalimbali katika hospital ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam nchini Tanzania inakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa dawa za kuwatibu watoto wenye ugonjwa huo.

Moja ya majengo ya hospitali ya taifa Muhimbili

Mkuu wa Idara ya Ustawi wa Jamii kutoka hospitali ya taifa ya Muhimbili, Bi. Beatrice Mugula na Meneja wa jengo la wodi ya watoto Bi. Prakiseda Chenge, wameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wakipokea msaada wa vifaa mbalimbali kutoka Benki ya Posta kwa ajili ya kuwahudumia watoto wenye saratani waliolazwa katika wodi hiyo.

Kwa upande wake Kaimu Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania Bi. Mystica Mapunda amesema huo ni utaratibu wa kawaida kwa benki hiyo kutoa misaada kwa jamii yenye mahitaji maalum.