Friday , 1st Dec , 2017

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christine Mndeme amefuta mkataba wa mkandarasi wa kampuni ya Rukolo kwa kushindwa kutimiza majukumu yake kwa wakati.

“Mkandarasi huyu wa kampuni ya Rukolo sitaki kumuona kwenye mkoa wa Ruvuma,  anapewa kazi katika Manispaa ya Songea mradi ambao ulitakiwa ukamilike June 30, 2017 na ni barabara ya urefu wa kilometa 8 zimemshinda”.

Aidha RC Mndeme ametoa wito kwa viongozi wa mkoa wa Ruvuma kutompa kazi tena mkandarasi huyo na tayari wameshafuta mkataba wake, kutokana na kusababisha wakazi wa wilaya ya songea kupata shida wakati wa kusafirii.

“Tumeshafuta mkataba naye na tumetangaza Tenda upya watu mbalimbali wameshatuma maombi, taratibu za kisheria zinaendelea ili apatikane mkandarasi mpya, ujenzi wa barabara hiyo ukamilike”.
 

Sikiliza Sauti hapo chini