Friday , 15th Apr , 2016

Wananchi wa Kijiji cha Magamba,Mkoani Katavi wamekana kushirikishwa katika uuzaji wa Ardhi wa hekari 45 kwa shilingi milioni 9 hatua ambayo Mkuu wa wilaya hiyo Paza Mwamlima kuamuru kukamatwa kwa aliekua mwenyekiti wa kijiji hicho.

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Paza Mwamlima

Mkuu huyo wa wilaya amesema amechukua hatua hiyo baada ya kuridhishwa kuwa Muhtasari uliotolewa na viongozi hao mwenyekiti wa zamani wa Kijiji Adrea Kitumba ulikuwa ni wa wa kughushi.

Wakiongea katika Mkutano huo baadhi ya Wananchi ambao majina yao yapo kwenye orodha ya walioshiriki katika uuzwaji wa Shamba hilo wamesema wanashangaa kuona majina hayo wakati hakuna aliewafata katika uandikishaji huo.

Mkuu huyo wa wilaya baada ya kuwasikiliza wananchi wa Kijiji hicho ndipo alipoamuru kutafutwa kwa viongozi wote waliohusika na suala hilo ambalo limeanza kuleta mgogor wa Ardhi katika eneo hilo.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Paza Mwamlima