Thursday , 17th Nov , 2016

Jumla ya shilingi millioni 400 zilitakiwa kutumika kukamilisha miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, vyoo na nyumba za walimu kwa shule nne Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro ifikapo mwezi desemba mwaka huu.

Licha ya pesa hizo kuwa tayari zimetolewa na wafadhili, mpaka sasa ni shule moja pekee yenye uhakika wa kukamilika kwa asilimia 99. 

Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilombero, Dennis Londo amesema kuwa miradi hiyo ambayo inafadhiliwa na Benki ya Dunia inatakiwa kukamilika Desemba 30 mwaka huu, lakini amewatupia lawama wakandarasi ambao wamepewa tenda hiyo kutokamilisha kwa wakati.

Kutokana na hali hiyo  Mkurugenzi huyo amesema kuwa endapo fedha hizo hazitatumika kwa muda uliopangwa fedha hizo zitarudishwa kwa mfadhili kitendo ambacho kitaisababishia serikali hasara kuanza kujenga miradi hiyo, wakati pesa zote zimeshatolewa na Benki ya Dunia.

Hata hivyo amesema kuwa serikali imeamua kufuatilia ujenzi wa miradi hiyo kuhakikisha kuwa kabla ya desemba 30 mwaka huu iwe imekamilika, ili wananchi wapate huduma ambayo inastahili.

Sikiliza hapa majibizano kati ya mkurugenzi na wakandarasi............