Mkuu wa mkoa wa Iringa Bi Amina Masenza
Mkuu wa mkoa wa Iringa Bi Amina Masenza amesema katika taarifa yake ya utekelezaji wa matokeo makubwa sasa kuwa Jumla ya wananchi 130,348 wanatarajiwa kunufaika na miradi ya maji inayoendelea kujengwa ambapo mpaka sasa wananchi wanaopata maji safi na salama ni 652278 sawa na asilimia 69.3.
Amesema kuwa utekelezaji wa mfumo wa matokeo makubwa sasa miradi iliyokamilika mpaka sasa ni miradi 10 katika vijiji 13 na inayoendelea kukamilishwa ni 14 katika vijiji 16 na ambayo haijaanza ni 7 katika vijiji 11.
Aidha ameeleza kuwa idadi ya vituo vilivyokamilika ni 149 na vinavyoendelea kukamilisha ni 232 na ambavyo havijaanza utekelezaji ni 141 hivyo idadi hiyo inafanya jumla ya miradi yote kuwa 522.
Hata hivyo jumla ya wanufaika ambao wanaoendelea kupata maji ni 30,787 na inayoendelea ili wanufaike ni 58,987 na kule ambapo miradi haijaanza itakapoanza watanufaika watu 40,574 na hivyo kufanya jumla ya wanufaika kuwa 130,348 endapo miradi yote itakuwa imekamilika.