Tuesday , 15th Apr , 2014

Jeshi  la  polisi  nchini  limetoa  donge  nono  la  shilingi  milioni  kumi  kwa  mwananchi  yeyote  atakayefichua  mtandao  wa  watu  wanaotengeneza  na  kulipua  mabomu  katika  mikusanyiko mbalimbali ya  wananchi.

Kamishna wa makosa ya jinai Tanzania Isaya Mngulu

Jeshi  la  polisi  nchini  limetoa  donge  nono  la  shilingi  milioni  kumi  kwa  mwananchi  yeyote  atakayefichua  mtandao  wa  watu  wanaotengeneza  na  kulipua  mabomu  katika  mikusanyiko  ya  wananchi  vitendo  ambavyo vimekuwa  vikiuwa  na kujeruhi  wananchi  wasio  na  hatia.

Hayo  yamesema  na  kamshina   wa  makosa  ya  jinai  nchini  (DCI)  Isaya  Mngulu  alipokuwa  akizungumza  na  waadishi  wa  habari  jijini   Arusha

Kuhusu   hatua  iliyofikiwa  kuwatafuta  watu  waliohusika  katika  tukio la  mlipuko  wa   bomu kwenye  baa  ya  Night Park  kamshna  Mngulu  amesema  hawajapatikana  na  kwamba  hata  waliohusika  kwenye  matukio  ya  bomu  katika  kanisa  la  Olasiti  na  pia  kwenye  mkutano  wa  CHADEMA Soweto  pia hawajapatikana  japo  amesema  jitihada  za  kuwatafuta  zinaendelea.

Katika hatua  nyingine  kamshina  Mngulu  amekiri  kuwa  changamoto  bado  ni  kubwa  katika  kuwatambua  watu  wanaoendesha  vitendo  hivyo  na  ameendelea  kuwaomba  wananchi  kusaidia  kwa  kutoa  taarifa   na  kwamba  hata  ndani  ya  vyombo  vya  dola  pia  iko  haja  ya  kujichunguza  kwani   haiwezekani  vitendeo  hivyo  viendelee  kutokea  na  wahusika  wasipatikane.

Wakizungumzia  vitendo hivyo   baadhi  ya  wananchi   wamelitupia   lawama  jeshi la polisi  kwa  kushindwa  hata  kutoa  taarifa  za  matukio  ya  milipuko  ya  mabomu  kila inapotokea.

Siku ya tarehe 13/04/2014 majira ya  saa  moja  na nusu   ulitokea  mlipuko  katika baa  ya Night Park  iliyoko  jijini  Arusha  uliojeruhi  watu  17  likiwa  ni  tukio la  tatu  kutokea  katika  jiji  la  Arusha  ambapo matukio  mengine  mawili  ya milipuko  ya  mabomu  yalitokea  mwaka  2013